WANANCHI wengi wa Taifa hili wamekuwa wakiuenzi utamaduni wao kwa kudumisha mila na desturi ,hivyo ingekuwa moja ya nchi zilizo kwenye orodha ya kusifika katika sanaa za utamaduni wao. Lakini
Tanzania haimo hata katika nchi zinazo sifika katika sanaa hiyo katika bara la Afrika na duniani kote ndani ya muugano wake wa bara na visiwani. Mwaadishi wa kujitegemea Twaha kivale anafafanua zaidi kuhusu kudidimia kwa utamaduni
Katika miaka ishirini na tatu iliyopita,kumekuwa na harakati nyingi za ukuzaji wa sanaa za maonyesho nchini mwetu na katika miaka hii ambapo vikundi vingi viliazishwa nje ya mfumo wa asili hususani mikoani .viliazishwa kwa madhumuni la kufanya biashara ya sanaa na kwahiyo kutoa ajira kwa wasanii.
Rakini sehemu kubwa ya vikundi hivi kwa sasa vimekufa,na vikundi vingine ambavyo vina jikongoja kwa kusuasua.Hata hivyo kuna vikundi vingine vipya kuendelea kuazishwa kwa nyakati tofauti.
Kwa wakati huu
Tanzania imeazisha mfuko wa utamaduni ilikuinua kiwango cha sanaa katika maigizo ya jukwaani,muziki wa asili,muziki wadansi na maigizo ya runinga (TV) ingawa hakuna wataalamu na walimu wa kutosha kuazia ngazi ya chini hadi juu ili kuwasaidia wasanii
katika mfumo wa ngoma za asili zimekuwa zikichezwa sana mijini katika vikundi mbalimbali lakini zikiwa tofauti na uasili wa utamaduni utakaotambulishwa kutokana na tofauti kubwa kati ya wachezaji wa asili wa ngoma za asili na wale wanaojifunza bila kuwa na asili.
Zamani sanaa ya utamaduni wa ngoma ya asili ilikuwa inachezwa kama burudani katika shughuli mbalimbali,watu walikuwa wakijionea bila kiingilio chochote na pia ilipo kuwa ina chezwa iliwashilikisha watoto na vijana wa likambalimbali
Baada ya uhuru hayati baba wa taifa letu (mimi ni Mtanzania), mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alitangaza kuendeleza utamaduni wetu hivyo sanaa ya ngoma iliendelezwa katika shule za msingi hadi vyuoni pia kulikuwa na vikundi mbalimbali kwa ngazi zote kuanzia kijiji hadi taifa
Vijana wengi wa
Tanzania wanamapenzi makubwa juu ya michezo ya kuigiza iwe ni jukwaani, redioni au kwenye hizi Luninga, na pia wana mapenzi kwa ngoma za asili ingawa hakuna walimu au wataalamu wa kuwafundisha kuanzia ngazi zote na hivyo kuwafanya kwenda ndivyo sivyo katika fani ya maigizo na kibaya zaidi kuna vikundi katika ngazi za chini wamekuwa wakielekezana wenyewe kwa wenyewa na hivyo kufanya sanaa hii kuigwa kwa kuona au kuigwa na wengine kwa uzoefu
Nchi hii imekuwa ikididimia katika sanaa ya utamaduni wa Kitanzania kuazia kipindi cha miaka ya tisini sababu ni kwamba hatuna ushindanishi wa vikundi uwe wa ngoma au maigizo na hivyo kufanya sanaa ya utamaduni kuzolota siku hadi siku.
Kwani kwa kufanya matamasha ya sanaa kwa kushindanisha vikundi kwa kila mwaka au mwezi kuna wafanya wasanii kubadilishana mawazo pia hata ujuzi na hivyo vikundi kuona kuwa wamefanya vizuri au vibaya katika maonyesho husika.
Katika matatizo ya maleba,ngoma na hali ya kifedha vikundi vingi vimekuwa vikifanya vibaya na kushindwa kuendeleza vikundi vyao na hivyo kufanya sanaa ya Tanzania kutotambulika ipasavyo Afrika na Duniani kote
Kwa matumizi ya jukwaani kama vile maleba,sauti,mwanga na mapambo mbalimbali ni muhimu ili kupendeza kwa mchezo na kueleweka kwa sanaa.inawezekana umuhimu na mahitaji yake katika mazingira ya kiasili si makubwa sana.Lakini kwa vikundi vinavyofanya shughulizao mijini ni muhimu .taaruma hii haijakomaa sana napia ipo hali ya kuipuuza katika shughuli zetu
Sasa ikiwa na viwango vya chini na kukosa uhakika hata wa kutambulika Afrika na Duniani katika maonyesho ya jukwaani mafanikio sasa yamebaki kuwa ni historia tu.
Kwa upande wa uigizaji wa runinga kwa sasa umeonyesha kujitahidi sana lakini tatizo bado lipo palepale kwa wataalamu hivyo kuna wafanya wasanii kuchanganya mchezo wa jukwaani,radioni,tv na vichekesho kuwa pamoja.
Taaluma ya msingi katika uwasilishaji wa tamthilia kwa hali ilivyo wasanii wengi wana upungufu ambao kwa upande mmoja unatokana na kutoelewa maana ya kuigiza na upande mwingine kutokuwa na stadi za kutosha za uigizaji.
Japo walaji wa bidhaa hii wamekuwa wakila vikiwa vibichi,yani wapezi wa sanaa ya maigizo wamekuwa wakilazimika kuangalia hivyo hivyo japokuwa mchezo huo haukupingwa picha vizuri,wachezaji(waigizaji)hawana uhusika na tatizo kubwa katika sanaa hii ni umri.
Kwani ukitangaza unataka wasanii wa maigizo ya kwenye tv ili kufanya tendo la upigaji wa picha
(shooting)basi watakao jitokezazaidi ni vijana wa miaka 17,19 hadi 25hawa watakuwa wengi zaidi hivyo mchezo kuufanya mchezo kutoeleweka yani Baba ni yupi na mtoto ni yupi.
Hakuna mbinu za kuwasaidia zaidi wasanii dhidi ya kuwa na walimu (wataalamu) hivyo kukosekana kwa walimu ni sababu zinazo tufanya tusiendelee kama inavyo takiwa na wataalamu walio maliza mafunzo yao hawajiungi na vikundi ili kuvisaidia katika maelekezo
Kwani tuna vyuo vingi vinavyo toa wahitimu kila mwaka wa fani hii ikiwemo Chuo cha Sanaa Bagamoyo ambacho kiliaza kutoa mafunzo mwaka 1981, programu ya mafunzo ya sanaa kwa walimu walio chini ya Wizara ya Elimu na utamaduni iliyo azishwa mwaka 1973katika chuo cha ualimu daresalama na baadae kuamishiwa butimba.
Vilevile kituo cha sanaa za maonyesho Tanzania (TZTC) kilichoazishwa mwaka 1998 kimeendesha warsha nyingi katika fani mbalimbali za sanaa za maonyesho lakini sanaa yetu bado imekuwa ikididimia kila siku,japokuwa wahitimu nao wana hitimu kila mwaka
Na kwa upande wa ngoma za asili vijana wanatakiwa kushilikishwa kikamilifu sababu bila kuwashilikisha ni kupoteza utamaduni wetu kwani baada ya miaka michache vijana watakuwa wakizifahamu tamaduni za wezetu ambao wali washilikisha vijana wao.tangu wakiwa wadogo
Kamanilivyo sema mwazo matamasha yanasaidia kujifunza ngoma au sanaa ya kabila lingine kwa kuona au kushiliki kwa kucheza tamaduni ambazo ni zahapahapa nchini kwani Tanzania ina makabila zaidi ya miamoja na ishilini (120)
Lakini sasa hivi tunaona vikundi vingi vinacheza ngoma za ubunifu ambayo haina uasili wa kitanzania na hivyo ni dalili za kupotea taratibu kwa tamaduni za asili na kuiga za kigeni kwa kisingizio cha ubunifu wakati Nchi za Ulaya wanapenda kuona utamaduni wa asili wa nchi husika.
Vikundi vya sanaa vya mijini vimekuwa vikicheza ngoma za asili tofauti na vile vya kijijini sababu ni kutokwenda vijijini na kukaa pamoja na wezao kisha wakajifunza aidha vikundi vya mjini vimekuwa vikiweka vionjo vya kisasa hivyo kupoteza uasili wa utamaduni huo.na hayo huwenda ndiyo yanayo changia kudidimia kwa sanaa nchini.
Inasadikiwa kwamba katika makabila hapa nchini yenye sauti nzuri wakati wa kuimba ni kabila la Wagogo na katika Afrika kabila hili lina shika nafasi yapili ambapo wakiongozwa na kabila la zulu toka afirika kusini kwa kushika nafasi ya kwanza
Pia kuna ngoma ya kabila kutoka wilaya ya uranga hii inaitwa sangula nayo inavionjo vinzuri sana na katika ngoma za makabila ambayo yanaweza kuwekwa kwenye rekodi ya kuitangaza
Tanzania basi hayo mawili ambayo ngoma zake na sauti zake zimeweza kufika nje ya nchi na kuitangaza kwa therusi ndogo.
Pia kabila la Wangoni limeweza kuitangaza
Tanzania na makabila kadha wa kadha tena kwa nguvu za mtu binafsi mmoja mmoja lakini ukisema watu wangine watasema na kubisha kwa maslahi yao tu.tena kwa kujingamba wakisema bila sisi wangefika huko.
Wakati vikundi vingi vimekuwa vikifurukuta kutafuta wafadhili ili waweze kuendesha shughuli za maonyesho ya jukwaani,kupiga picha za maigizo ,maleba na ngoma hapo ndipo wanapo jikuta wanakandamizwa kima pato aidha vikundi kuishia sifa ya kufanya vinzuri au kupewa hera kidogo kwa wasanii na fedha zote anabakinazo mfadhili.
Na kibaya zaidi ni kwamba wafadhili wengi hujitokeza kwenye vikundi kwa manufaa yao ya kibiashara au kimapato na wasanii wanabaki bila fungu lolote na hivyo huwakatisha tamaa wasanii pia hutawanyika na kutafuta makundi mengine nahivyo hudidimiza sanaa ya
Tanzania
Wasanii wengi wa Tanzania wanaamini kwamba watafanikiwa hata kama hawana wataalamu au wafadhili,sababu ya kuamini ni kuwa wao ni wasanii na sanaa ipo ndani ya damu yao hivyo wakidhani kuzungusha kiuno sana au kuwa msemaji sana ndivyo sanaa inavyo taka
katibu wa kikundi cha zabibu Idrissa magomeni kilichopo mkoani Dodoma alisema kuwa“Tungefanikiwa kama wahusika wangetuletea walimu kutoka bagamoyo na kutoa mafunzo kwa vikundi vya vijana wengi wenye vipaji ambao nawaona wamejikusanya huku mitaani tena wenye vipaji”
Leo sanaa nchini imeachwa kwa wasanii wenyewe na imekuwa ikitumika na wanasiasa katika makujukwaa pia mafunzo kwa wasanii si kitukilichowekewa mipango maalumu ingawa vikundi vimeoneka kutokuwa na walimu wenye taaluma ya sanaa.
Kama nilivyo gusia mwanzo kuwa serikali ya Tanzania imeazisha mfuko wa utamaduni ambao utasaidia vikundi vya sanaa hapa nchini japokuwa vikundi vingi havina taalifa ya kutosha juu ya swala hili na baadhi havijasajiliwa katika baraza la sanaa la taifa
Serikali isipoangalia swala hili kwa makini itakuwa imeazisha mradi kwa watu ambao ndio waliiangusha au kuendelea kuangusha utamaduni wa Tanzania,siyo maanayangu kumtafuta mchawi wa sanaa
Ila maanayangu ni kuangalia watanzania wanainua sanaa yao na kuitangaza kwa nguvu zote ndani na nje ya nchi na kama itakuwa nimemgusa mtu yeyote basi ajue ni mchango wangu tu wa mawazo katika kuinua sanaa ya Tanzania
Baadhi ya viongozi wa vikundi wamekuwa wao ndio wenyeviti ,makatibu wa vikundi na waweka hazina,watuzi na walimu wa kikundi,pia kuna baadhi ya maafisa utamaduni wengine wamekuwa wakishabikia vikundi fulani kwa maslai yao binafsi.
Hapa nachotaka kusema nikwamba ikitokea kazi fulani ya kampeni mfano maralia,kipindupindu au kampeni ya ukimwi si kituchaajabu ukaona kina kwenda kikundi fulani ambacho huwa kinakwenda katika shughuli zingine zote zinazo tokea hapo mkoani au wilayani
Na ukiangalia utaona kuna vikundi vingine,lakini kwanini havikwenda au huwa haviendi jibu utaona nikushabikia kwa baadhi ya maafisa utamaduni tena ushabiki huu hufanya kuchukua vikundi visivyo na sifa wala uwezo kisanii tena havija sajiliwa katika baraza la sanaa
Kwa hiyo kwa watu kama hawa kuendelea kuwepo madarakani ndio jambo baya kwa sanaa yaTanzania sababu wao ndio kizuizi cha maendeleo ya sanaa na nikikwazo kikubwa kwa wasanii ambao wanafurukuta katika kuendeleza sanaa kujiendeleza kiusanii
Kama nilivyo gusia hapo mwazo kwa baadhi ya maafisa utamadani kushabikia vikundi kuta pelekea uwezekano hata kuazisha vikundi ili kuombea fedha katika mfuko wa utamandu au kupendekeza kikundi shabiki kuwezeshwa kwa ajili ya manufao yao binafsi
Tanzania imeshindwa kuwa na utaalamu ambao nchi nyingine za Afrika zimekuwanao mfano kama naigeria,Uganda ,Kenya na nchi zingine kadha wa kadha kwa sababu ya kutofuaata utaratibu mdogo hinyo ni kupinga na kuweka shinikizo hizi za mfumo mbaya
Sanaa za maonyesho lazima iongozwe na maafisa waliobobea katika sanaa na mafunzo kwani hii ni taaluma na wasishabikie vikundi kwani kwa kufanya hivyo ni kuwakatisha tamaa wasanii wengine
Kwahiyo tumeanzisha mfuko wa utamaduni kama mfumo wa kuendeleza sanaa ya Tanzania kama kipaumbele chetu kwa kipindi cha miaka inayokuja kwani nina uhakika kwamba tukizingatia baadhi ya matatizo ya wasanii na kuyatatua tutaiwezesha Tanzania kuingia katika matangazo na kufahamika katika Afrika na Duniani
alamsiki